...

Jamii Voice Media

Sauti ya Wasio na Sauti!”

Our Story

DIRA YETU Kujenga jamii ya Kitanzania iliyo salama, yenye usawa wa kijinsia, inayopinga ukatili wa kijinsia kwa vitendo, na inayostawi kwa misingi ya haki, amani, na fursa sawa kwa wote. DHAMIRA YETU Kuwa chombo makini cha habari na elimu ya kijamii kinachochochea mabadiliko chanya katika jamii kwa kutoa taarifa, kuelimisha na kushawishi sera zinazolenga kutokomeza ukatili wa kijinsia na kukuza usawa wa kijinsia nchini Tanzania. MALENGO YETU MAHUSUSI 1. Kuelimisha jamii kuhusu haki na usawa wa kijinsia kwa kutumia vipindi vya redio, makala, video fupi, na kampeni za mitandaoni zitakazowalenga vijana, wanawake, wanaume, na watoto. 2. Kuwezesha wanawake na wasichana kupata uelewa na ujasiri wa kushiriki katika maamuzi ya kijamii na kisiasa kupitia maudhui yanayojenga uwezo na kuonesha mifano ya wanawake waliowezeshwa. 3. Kushirikiana na watunga sera, viongozi wa dini, na wadau wa maendeleo ili kuibua mijadala ya kina na kutoa mapendekezo ya kisera juu ya kuzuia ukatili wa kijinsia na kuboresha mazingira ya usawa wa kijinsia. 4. Kupaza sauti za manusura wa ukatili wa kijinsia na kuzigeuza kuwa nyenzo ya mabadiliko kwa kutumia majukwaa salama ya kutoa simulizi zao kwa lengo la kuleta uelewa, huruma, na hatua za kijamii. 5. Kufanya tafiti na uchambuzi wa taarifa kuhusu hali ya usawa wa kijinsia na ukatili wa kijinsia kwa lengo la kutoa ripoti na mapendekezo yatakayosaidia sera na mipango ya kitaifa na ya kijamii. 6. Kuendeleza mafunzo na semina kwa waandishi wa habari na wanaharakati wa jamii ili kuwawezesha kuripoti kwa weledi kuhusu masuala ya kijinsia na haki za binadamu.

Our Values

Empathy

Lorem ipsum dolor sit amet consectetur adipisicing elit. Quaerat quisquam aperiam. elit. Quaerat quisquam aperiam

Integrity

Lorem ipsum dolor sit amet consectetur adipisicing elit. Quaerat quisquam aperiam

Teamwork

Lorem ipsum dolor sit amet consectetur adipisicing elit. Quaerat quisquam aperiam

Excellence

Lorem ipsum dolor sit amet consectetur adipisicing elit. Quaerat quisquam aperiam