TGNP yaendesha utafiti raghibish Mgagao Mwanga


TGNP yaendesha utafiti raghibish Mgagao Mwanga

By Deogratius Temba

February 3, 2025

ยท       Wanachi Mgagao Mwanga wana na mapendekezo

Na Deogratius Koyanga

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), umewawezesha wananchi kutoka kata ya Mgagao, Halmashauri ya Wilaya ya mwanga, Mkoani Kilimanajro kuendesha zoezi la utafiti uraghibish ili kutokomeza vitnedo vya Ukatili wa Kijinsia na kukuza usawa wa Kijinsia.

 Zoezi hilo ni sehemu ya mradi wa  Kuvunja vikwazo: kuondoa na kutokomeza Ukatili wa Kijinsia na Kukuza usawa wa Kijinsia  unaotekelezwa na TGNP katika halmashauri hiyo. Ambapo jamii imejengewa uwezo namna ya kuibua, kuchambua na kuweka mikakati ya utatuzi wa changamoto zinazowazunguka kwa kuhsirikiana na viongozi katika ngazi mbalimbali.

 Miongoni mwa changamoto za ukatili wa kijinsia zilizoibuliwa ni pamoja na Suala la kushamiri kwa vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kama vile Ubakaji kwa wanawake hasa wasichana, mimba za utotoni, ukeketaji wa wasichana na kuongezeka kwa uporaji wa mali hasa mifugo.

Katika mapendekzo yao, washiriki wa uraghibish huo, walipendekza kwamba;

Halmashauri iweke sheria kali za vijiji na wasimamizi wa sheria (Polisi na mahakama) na vyombo vingine zifanye kazi kwa uadilifu ili sheria itekelezeke. Halmashauri isimamie mchakato wa uandaaji wa bajeti uwe shirikishi kuanzia ngazi za kijiji ili tuwe na bajeti yenye mrengo wa Kijinsia itakayogusa mahitaji ya kila kundi.

Kuuhuisha kamati za Ulinazi wa Mama na Mtoto (MTAKUWWA) katika kata na vijiji vyote, zitambue majukumu yake na mfumo wa uwajibikaji yaani ziwe na taarifa zake za utekelezaji.

Mwongozo wa serikali (Feb. 2022) wa kuwarudisha wanafunzi walioacha masomo kwa sababu mbalimbali uanze kutumika ndani ya Kata. Mratibu Elimu Kata (MEK) aanze kuwabaini wasichana walioko mitaani na kuwarudisha shuleni kwa mujibu wa mwongozo.

Halmashauri isaidie usimamizi  na utekelezaji wa sheria ndogo ambazo zitathibiti watoto wa shule kuzurura hovyo siku ya Ijumaa mnadani na katika  magenge na kwenye vibanda vya kuoneshea Video.

Sheria kali zichukuliwe dhidi ya kutokomeza Mimba na ndoa za utotoni. Maafisa Ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii washirikiane na dawati la Jinsia na Mtoto-Polisi, kuharakisha kesi za ubakaji na wanaobainika wahukumiwe kwa mujibu wa sheri zetu.

Halmashauri isimamie watendaji wa Vijiji kufanya mikutano ya kisheria ya vijiji sambamba na mikutano maalum ya kuibua na klujadili vipaumbele vya Bajeti au miradi ya maendeleo (Mchakato wa uibuaji wa fursa na vikwazo katika maendeleo-[O&OD]. Ili kuweka kipaumbele masuala muhimu kama haya ya maji, mabweni nk.

Mradi wa umeme wa REA wa Kijiji cha Pangaro, uweke kipaumbele kwenye shule za msingi, zahanati  ili kuboresha huduma na kuwavutia watumishi kufanya kazi katika maeneo hayo

Kuendelea kushirikiana kati ya jamii na serikali kutoa elimu na kuzuia vitendo vya Ukeketaji katika jamii ya Mgagao hasa vitongoji vinavyotajwa kuwa na mila hizo.