Maoni na mapendekezo ya Jamii kuhusu Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26


Maoni na mapendekezo ya Jamii kuhusu Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26

By Deogratius Temba

March 19, 2025

MTANDAO WA JINSIA TANZANIA (TGNP)

WASILISHISHO LA SEMINA ZA JINSIA NA MAENDELEO (GDSS) MACHI 19,2025.

Mwasilishaji: Deogratius Temba, Mchambuzi wa Bajeti kwa mtazamo wa Kijinsia

 

Mwelekeo bajeti 2025/26

 

Serikali ya Tanzania imependekeza bajeti ya shilingi trilioni 55.06 kwa mwaka wa fedha 2025/26, ikiwa ni ongezeko la asilimia 13.4 ikilinganishwa na bajeti ya shilingi trilioni 50.29 ya mwaka 2024/25.

VIPAUMBELE VYA BAJETI YA TANZANIA KWA MWAKA 2025/26 (Kama ilivyowasilishwa kwenye mapendekezo ya bajeti Machi 2025)

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imependekeza bajeti ya shilingi trilioni 55.06 kwa mwaka wa fedha 2025/26, ikiwa ni ongezeko la takriban asilimia 13.4 kutoka bajeti ya mwaka 2024/25.(Gazeti la Mwananchi la tarehe…)

Vipaumbele Vikuu vya Bajeti ya 2025/26 ni pamoja na

1. Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2025

  • Kuwezesha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika maandalizi na uendeshaji wa uchaguzi mkuu.
  • Kutoa elimu ya mpiga kura na kuhakikisha ushiriki wa makundi yote (wanawake, vijana, watu wenye ulemavu)

2. Ulipaji wa Deni la Taifa

  • Bajeti kubwa imeelekezwa katika kulipa madeni ya ndani na nje ili kulinda ustahimilivu wa kiuchumi.
  • Hatua hii inalenga kuimarisha uaminifu wa serikali kwenye masoko ya fedha.

3. Uwekezaji katika Sekta ya Uzalishaji

  • Kuongeza uzalishaji wa viwandani na kilimo chenye tija.
  • Kukuza biashara na mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje.
  • Kuboresha viwanda vya kuongeza thamani kwa mazao ya kilimo.

4. Miundombinu ya Uchumi na Kijamii

  • Kuendeleza ujenzi wa barabara, reli, bandari, na miundombinu ya nishati (umeme).
  • Kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama vijijini na mijini.

5. Elimu na Afya

  • Uboreshaji wa elimu ya awali, msingi, sekondari na vyuo kwa kuongeza walimu, vifaa, na madarasa.
  • Kuboreshwa kwa huduma za afya, upatikanaji wa dawa, na ujenzi wa zahanati/vituo vya afya.

6. Kujenga Uchumi Shindani na Shirikishi

  • Kuwezesha vijana na wanawake kiuchumi kupitia mikopo na programu za ujasiriamali.
  • Kupunguza ukosefu wa ajira kwa kukuza sekta binafsi.

7. Ulinzi na Usalama

  • Kuimarisha amani, usalama wa raia, na mipaka ya nchi.
  • Kuboresha mazingira ya utawala bora na haki za binadamu.

8. Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira

  • Kuwekeza katika miradi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
  • Kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji.

9. Mageuzi ya Kisera na Kiutawala na kukuza usawa wa Kijinsia na uwezeshaji wa wanawake na makundi maalum

  • Kuendelea na mageuzi katika mifumo ya kodi, usimamizi wa fedha za umma na matumizi ya TEHAMA serikalini.
  • Kukuza usawa wa Kijinsia, uwezeshaji wa wanawake na makundi maalum kiuchumi.

 

UTEKELEZAJI WA BAJETI 2024/25

Hadi kufikia Oktoba 2024 (robo ya kwanza) ya mwaka wa fedha 2024/25 fedha zilizokusanywa ni shilling Trilion 11.5.

BAJETI YA MWAKA 2025/26

Makadirio ya bajeti ni shilling Trilion 55.06, ambapo Mapato ya ndani ni 38.9 Trilion , ukilinganisha na Shiling Trilion 34.6 kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Kati ya Bajeti nzima ya shs. 55.06 Trilion matumkzi ya Kawaida ni shs. 38.6, wakati Bajeti ya maendeleo ni shilling Trilion 16.4. ambapo kati ya bajeti nzima shilling Trilion 40.09 (69.7%) ni fedha na makusanyo ya ndani, wakati shilling Trilion 16.07 (30.3%) ni fedha za wahisani, misaada, mikopo nafuu,  kutoka nje).

Tofauti ya Bajeti hii ya mwaka 2025/26 ya Trilion 55.06, na Bajeti ya mwaka 2024/26 ni asilimia 13.. Yaani kuna ongezeko la asalimia 13. Tunapaswa kuendelea kujiuliza, hii 13% inaenda kuboresha nini kipya?  Je tutaendelea kubaki kama tulivyokuwa? Je ongezeko hili linagusa maisha ya mwananchi wa kawaida?

Jedwali (Table) linaloonesha muhtasari wa Bajeti ya Taifa ya Tanzania kwa mwaka wa fedha 2025/26:

Maelezo

Kiasi (TZS Trilioni)

Asilimia (%)

Jumla ya Bajeti

55.06

100%

Mapato ya Ndani

38.9

70.6%

Fedha kutoka nje (misaada/mikopo)

16.07

29.4%

Matumizi ya Kawaida

38.6

70.1%

Matumizi ya Maendeleo

16.4

29.9%

Ongezeko kutoka 2024/25

13%

Maswali ya kuzingatia:

  • Je, ongezeko la bajeti ya 13% linaakisi maboresho ya maisha ya mwananchi wa kawaida?
  • Je, fedha hizi zinagusa sekta zenye changamoto kubwa kama afya, elimu, maji na uwezeshaji wanawake?

 

 

MAPENDEKEZO YENYE MTAZAMO WA KIJINSIA KATIKA BAJETI YA 2025/26

1. Kuweka fedha mahsusi kwa ajili ya kutekeleza Sheria, Sera, na Mipango ya Kitaifa ya Usawa wa Kijinsia

  • Mfano: Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2022/23–2026/27).
  • Bajeti ya kutosha itolewe kwa Mikoa na Halmashauri kutekeleza miongozo hii.
  • Tutahitaji kusikia serikali kupitia bajeti zake za wizara na Bajeti kuu wakieleza jinsi ambavyo kuna fedha zimetengwa kutatua changamoto za Ukatili wa Kijinsia

2. Kuongeza Bajeti ya Miradi Inayowalenga Wanawake Kiuchumi

  • Fedha zaidi zielekezwe katika:
    • Uwezeshaji wanawake wajasiriamali (kupitia mifuko ya wanawake, vijana na walemavu).
    • Mafunzo ya stadi za kazi kwa wanawake na wasichana.
    • Masoko na mitaji kwa wanawake wa vijijini na mijini.
  • Halmashauri zianzishe na kuendeleza vituo rafiki vya wanawake wajasiriamali (one stop centers).

3. Kuweka Ruzuku kwa Huduma za Unpaid Care Work

  • Bajeti itambue na kuwekeza katika huduma kama:
    • Huduma za kulea watoto (day care centres).
    • Huduma za afya ya wazee na watu wenye ulemavu.
  • Kupunguza mzigo wa kazi zisizolipwa unaowakumba wanawake na kuzuia ushiriki wao kwenye siasa na uchumi.
  • Kufuta kodi au kuweka ruzuku kwenye gesi ya kupikia. Makampuni yanayosambaza gesi yasambaze kwa bei rafiki ili kumtu Mama kuni kichwani kwa kuhakikisha wanawake wote wananufaika na gesi na kuacha kabisa matumizi ya kuni na mkaa
  • Kutenga fedha na kuweka ruzuku ya afya kwenye Bima ya afya kwa wote “Kusiwepo na matabaka kwenye Bima ya afya” iwepo Bima moja kwa wote ambayo kila mwananchi atatibiwa vizuri na kwa bei nafuu

4. Kuweka Bajeti kwa Ajili ya Kuzuia na Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (GBV)

  • Kutenga fedha kwa ajili ya:
    • Ujenzi na uendeshaji wa vituo rafiki kwa waathirika wa GBV.
    • Mafunzo kwa polisi, mahakimu, na watumishi wa afya kuhusu usaidizi wa manusura wa ukatili.
    • Elimu kwa jamii kuhusu athari za ukatili wa kijinsia.
  • Zile halmashauri ambazo hazina madawati ya jinsia au huduma kwa waathirika wa GBV zianze kuyatengeneza mwaka huu.

5. Kuweka Bajeti ya Kuongeza Ushiriki wa Wanawake Katika Uongozi na Maamuzi

  • Kufadhili kampeni za elimu ya uraia kuhusu ushiriki wa wanawake kwenye uchaguzi mkuu 2025.
  • Kuwajengea uwezo wanawake wagombea kupitia semina, mentorship, na mitandao ya wanawake viongozi.
  • Kuhakikisha wanawake wanashiriki kwenye mabaraza ya ardhi, kamati za shule na miradi ya maendeleo.

6. Kuimarisha Takwimu za Jinsia (Gender-Disaggregated Data)

  • Bajeti itumike kuwezesha ukusanyaji wa takwimu zinazotenganisha wanawake, wanaume, vijana, na watu wenye ulemavu kwenye sekta zote.
  • Hii itasaidia kupanga na kupima athari ya miradi ya serikali kwa makundi tofauti ya kijamii.

7. Kuainisha Bajeti Yenye Mtazamo wa Kijinsia (Gender Responsive Budgeting - GRB) Kwenye Sekta Zote

  • Wizara na Halmashauri zote zianze kuandaa mipango na bajeti zinazoonyesha wazi mchango kwa usawa wa kijinsia.
  • Mfano: Sekta ya Kilimo iweke bajeti ya teknolojia zinazosaidia wanawake (kama mashine za kuchakata mazao), Sekta ya Afya izingatie afya ya uzazi, nk.

 

Karibuni kwa Majadiliano: Je nini matamanio yetu? Tunatarajia kuona nini sisi kama wanajamii?