Mdahalo wa TGNP waisukuma RUWASA kupeleka maji sekondari ya Mgagao


Mdahalo wa TGNP waisukuma RUWASA kupeleka maji sekondari ya Mgagao

By Deogratius Temba

March 18, 2025


Na mwandishi wetu

KUTOKANA  na shida kubwa ya ukosefu wa maji safi na salama katika shule ya sekondari Mgagao, wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, linasababisha kushukja kwa kiwango cha ufaulu na kusababisha utoro, hadha hiyo inaenda kutatualiwa hivi karibuni

Akizungumza na timu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), iliyokuwa katika zoezi la utafiti raghibishi katika kata hiyo, Mhandisi wa Maji wa Ruwasa Wilaya ya Mwanga, Samweli….. alisema kwamba, taasisi hiyo itahakikisha majhi yanafika katika shule hiyo sambamba na sehemu nyingie za vijiji vya kata hiyo

Mradi wa maji wa Mwanga, Same hadi Korogwe (MSK) unapita katika kata hiyo ilihali ikiwa haina kabisa chanzo cha uhakika cha maji , tofauti na visima viwili vilivyoko katika msikiti wa Mgagao na Kanisa Katoliki Mgagao.


Shule ya sekondari ya Mgagao, yenye idadi ya wanafunzi…… haina kabisa chanzo chochote cha maji, hali inayotishia afya za wanafunzi na waalimu pamoja na kusababisha watoto kuachelewa kufika shuleni na au kutoroka kutokana na kulazimishwa kubeba maji angalau lita 3 kila siku ambayo pia nyumbani hayapo.

Azkiungumza na timu ya TGNP katika chanzo kipya cha kuchotea maji kilichopo katika kijiji cha Mgagao, Mhansisahi alisema…. NImekuja hapa kuangalia hali ya upatikanaji wa maji hapa, sisi ofisi yetu tunatambua tatizo hili. Tuna mipango na hili eneo, na sasa hivi ninaelekea sekondari ya Mgagao kuzungumza n Mkuu wa shule ili tuwapelkee wanafunzi maji” alisema Mhandisi……..

Zoezi la uraghibish katika Kata hiyo, lililoendeshwa na TGNP, sambamba na Mdahalo wa Jamii uliofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari  suala la maji liliibuliwa na kuonekana ni tatizo kubwa linalokwamisha maendeleo na linasababisha kwa kiasi kikubwa kukidhiri kwa vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kama ubakaji, ulawiti, vipigo, mifgogoro ya ndoa, mimba za utotoni na rushwa ya ngono.